Millionaire  Ads

Sunday, May 11, 2014

Tuwatazame wanyama wadogo wadogo kama nyani

Tags
Siku zilizopita tuliangala wanyama watano ambao hutambulika kama big five.Wiki hii tutawatazama wanyama wadogo wote hasa tutaanza na baboon.Watu wa mbugani humwita sharobaro kutokana na mwendo wake wa madaha mtazame huyu hapa

Tuesday, May 6, 2014

Tumtazame nyati na tabia zake

Tags


Tumtazame nyati au mbogo kwa kifupi' Wengi humwita mbogo na kweli anatisha ukimuuzi.Mnyama huyu kwa jina zuri waweza mwita ng'ombe pori anasifa na ufanano kama wa ng'ombe.

Nyati ana urefu wa 140-170sm

Pia uzito wa dume ni 785kg jike anauzito wa,715kg Nyati anatunza mimba miezi 11 Anauwezo wa kuzaa mtoto mmoja tu na si zaidi Pia anauwezo wa kuishi miaka 23 

MAKUNDI YAO 1)Gregarsus& 2)Teritorial home range fuatana nami katika page hii ili upate kujua maisha yake kuzaliwa hadi kufa

Monday, May 5, 2014

Mfahamu mnyama kifaru au faru kama wengine mnavyomwita

Tags
Kifaru ni miongoni wa wanyama watano wanaounda kundi la BIG FIVE ONA SIFA ZAKE Anaurefu wa sm 135-230 na anatunza mimba mda wa miezi 15

MAKUNDI YAO Kama ilivyo kwa wanyama wengine kifaru wapo katika makundi haya mawili 1)Solitary group 2)Cals group 

MAKAZI YAO Wanapatikana maeneo ya WOODLAND 

AINA ZA HAWA FARU 1)Faru weupe ambao hupatikana Afrika ya kusini na North-werst Uganda 2)Faru Weusi hawa hupatikana tanzania na kenya.

 TUTAKUJA ANGALIA MATUMIZI YA PEMBE YA FARU Bara la Asia waliamini pembe ya Faru hasa uloto wake kuwasaidia nguvu za kiume je kwa Tanzania na Nchi nyingine hutumiaje? usikose kufuatilia mada hii 
Huyu ni kifaru


Mtazame chui akiwa amekaa juu ya mti akiangalia windo.

Tags
Swali: unajua chui huwinda usiku.Sababu gani hufanya awindi mda huo? Pia kwanini akiuwa mnyama mla nyama hali nyama yake? unajua jina wamwitalo watu wa mbugani? kama simba huitwa sharubu chui je? Fuatana nami kujua maisha ya chui kwenye website hii kila siku.


Chui akiwa kwenye mti akiangalia windo

Mjue chui 
REPRODUCTION Jike hutunza mimba mda wa siku 105-110 na anauwezo wa kuzaa watoto wawili hadi wanne na si zaidi. 

BAREHE YAO Dume hubarehe akiwa na umri wa mwaka mmoja wakati jike hubarehe atimizapo umri wa mwaka 1.5.watoto wa chui huanza kula nyama watimizapo umri wa miezi sita 

UMRI WA KUISHI Chui huwa na uwezo wa kuishi miaka 15-18 kama hajapatwa na maradhi 

UWINDAJI Hatua ambazo hutumia Simba ndizo azitumiazo Chui.Kama ulinifuatilia kwenye Simba nazani ushazifaham 

MAKUNDI YAO 1) Family 2)Mating pear 

SEHEMU WANAKOPATIKANA Jihadhari maeneo haya unapokuwa mbugani 1)Misitu minene 2)vichakani 3) Maeneo yaliyojificha 

UZITO WAO Jike anauzito wa kg 60-75 Dume anauzito wa 90kg 

SPEED ZAO Chui hukimbia umbali wa 112km kwa saa huyu anaweza akama mnyama mwenye mbio za ajabu. Kama unafuatilia website hii nitakuja kupa tofauti ya chui na duma wengi hushindwa kutofUtisha

Thursday, May 1, 2014

Sheria za National Park

Tags

Wengi hunipigia simu kutaka ufafanuzi hasa ya watu wanaoishi mbugani inakuwaje?
Edward Mtega
nimependa swali hilo kabla ya kuwajibu naombeni muwe mnatoa maoni humu kwenye blog hii itasaidia sana: UFAFANUZI Leo niwaelezee camp ya tandala iliyopo national park ya luaha mkoani iringa.Camp hii hadi sasa inamiaka 12 na zaidi ni camp pekee ambayo inawafanyakazi wa jinsia zote wakati camp nyingine huchukua wafanyakazi wa kiume tu.Kutokana na sifa ya camp hii ya tandala wageni wengi kutoka bara la ulaya,asia na america huja kwa wingi kutokana na sababu zifuatazo: kwanza: mahema bora na yenye viwango vya kimataifa ambayo ndani kuna maji ya moto,solar,vitabu,choo,bafu,pamoja na madirisha yenye uundo wa neti ya zipu inayoruhusu kumwona mnyama akipita. Pili:gari za imara za kuwatembeza wageni pamoja na matoure guide waliobobea katika masuala ya pori Tatu:working safari utalii wa miguu ndani ya mbuga mgeni akiwa anaongozana na masai kwa ulinzi wake hii watalii hupenda hasa siku wanapokaribia kuondoka huomba kwenda kwenye maboma ya umasaini: Ushauri kama umefanikiwa kwenda kutarii jihadhali na vitu vifuatavyo:

1)kuchukua mabaki ya wanyama kama mavi ya tembo,fuvu,nk 2)kuwapa wanyamapori vyakula anavyokula bibadamu mfano:kumpa nyani ndizi,pipi ni kosa la jinai 3)kupiga kelele hasa unapokuwa mbugani au kupiga honi za magari ni kosa unaweza fanya wanyama kupaniki 4)kwenda na pikipiki au na wanyama wa kufugwa hairuhusiwi 5)kuwasha moto 6)kula au kuwinda wanyama pori ukishikwa utaratibu unaufahamu 7)huruhusiwi kutembea mbugani au kuokota au kurina au kuvua samaki pasipo kibari maalumu, kwa kifupi mtakuwa mmeelewa sheria za park






Picha hii nimekaa na huyu masai anaitwa maimbura yeye na masai mwenzake anaitwa kijangwaa ni masai waweza sema wa ajabu kwani hufika mda hucheza na tembo kitu ambacho si cha kawaida pia wamenusurika na simba mara,nyingi.Wageni huwapenda na hata bosi wao! tukipata mda nitawasimulia mikasa ya hawa jamaa