Millionaire  Ads

Thursday, May 1, 2014

Sheria za National Park

Tags


Wengi hunipigia simu kutaka ufafanuzi hasa ya watu wanaoishi mbugani inakuwaje?
Edward Mtega
nimependa swali hilo kabla ya kuwajibu naombeni muwe mnatoa maoni humu kwenye blog hii itasaidia sana: UFAFANUZI Leo niwaelezee camp ya tandala iliyopo national park ya luaha mkoani iringa.Camp hii hadi sasa inamiaka 12 na zaidi ni camp pekee ambayo inawafanyakazi wa jinsia zote wakati camp nyingine huchukua wafanyakazi wa kiume tu.Kutokana na sifa ya camp hii ya tandala wageni wengi kutoka bara la ulaya,asia na america huja kwa wingi kutokana na sababu zifuatazo: kwanza: mahema bora na yenye viwango vya kimataifa ambayo ndani kuna maji ya moto,solar,vitabu,choo,bafu,pamoja na madirisha yenye uundo wa neti ya zipu inayoruhusu kumwona mnyama akipita. Pili:gari za imara za kuwatembeza wageni pamoja na matoure guide waliobobea katika masuala ya pori Tatu:working safari utalii wa miguu ndani ya mbuga mgeni akiwa anaongozana na masai kwa ulinzi wake hii watalii hupenda hasa siku wanapokaribia kuondoka huomba kwenda kwenye maboma ya umasaini: Ushauri kama umefanikiwa kwenda kutarii jihadhali na vitu vifuatavyo:

1)kuchukua mabaki ya wanyama kama mavi ya tembo,fuvu,nk 2)kuwapa wanyamapori vyakula anavyokula bibadamu mfano:kumpa nyani ndizi,pipi ni kosa la jinai 3)kupiga kelele hasa unapokuwa mbugani au kupiga honi za magari ni kosa unaweza fanya wanyama kupaniki 4)kwenda na pikipiki au na wanyama wa kufugwa hairuhusiwi 5)kuwasha moto 6)kula au kuwinda wanyama pori ukishikwa utaratibu unaufahamu 7)huruhusiwi kutembea mbugani au kuokota au kurina au kuvua samaki pasipo kibari maalumu, kwa kifupi mtakuwa mmeelewa sheria za park






Picha hii nimekaa na huyu masai anaitwa maimbura yeye na masai mwenzake anaitwa kijangwaa ni masai waweza sema wa ajabu kwani hufika mda hucheza na tembo kitu ambacho si cha kawaida pia wamenusurika na simba mara,nyingi.Wageni huwapenda na hata bosi wao! tukipata mda nitawasimulia mikasa ya hawa jamaa







EmoticonEmoticon